21 Hakikusalia kitu asichokula;Kwa hiyo kufanikiwa kwake hakutadumu.
22 Katika kujaa kwa wingi wake atakuwa katika dhiki;Mkono wa kila anayesumbuliwa utamjia.
23 Hapo atakapo kulijaza tumbo lake,Mungu atamtupia ukali wa ghadhabu zake,Na kuunyesha juu yake akiwa anakula.
24 Ataikimbia silaha ya chuma,Na uta wa shaba utamchoma kwa pili.
25 Yeye autoa, nao watoka mwilini mwake;Naam, ncha ing’aayo yatoka katika nyongo yake;Vitisho viko juu yake.
26 Giza lote linawekwa kwa ajili ya hazina zake;Moto ambao haukuvuviwa na mtu utamla;Utayateketeza yaliyosalia hemani mwake.
27 Mbingu zitafunua wazi uovu wake,Nayo nchi itainuka kinyume chake.