24 Ataikimbia silaha ya chuma,Na uta wa shaba utamchoma kwa pili.
25 Yeye autoa, nao watoka mwilini mwake;Naam, ncha ing’aayo yatoka katika nyongo yake;Vitisho viko juu yake.
26 Giza lote linawekwa kwa ajili ya hazina zake;Moto ambao haukuvuviwa na mtu utamla;Utayateketeza yaliyosalia hemani mwake.
27 Mbingu zitafunua wazi uovu wake,Nayo nchi itainuka kinyume chake.
28 Maongeo ya nyumba yake yataondoka,Yatamwagika mbali katika siku ya ghadhabu zake.
29 Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu itokayo kwa Mungu,Na urithi aliowekewa na Mungu.