5 Ya kuwa shangwe ya waovu ni kwa muda kidogo,Na furaha ya wapotovu ni ya dakika moja tu?
6 Ujapopanda ukuu wake mpaka mbinguni,Na kichwa chake kufikilia mawinguni;
7 Hata hivyo ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe;Hao waliomwona watasema, Yuko wapi?
8 Ataruka mfano wa ndoto, asionekane;Naam, atafukuzwa kama maono ya usiku,
9 Jicho lililomwona halitamwona tena;Wala mahali pake hapatamtazama tena.
10 Watoto wake watataka fadhili kwa maskini,Na mikono yake itarudisha mali yake.
11 Mifupa yake imejaa ujana wake,Lakini utalala nchi naye mavumbini.