1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,
2 Yasikizeni sana maneno yangu;Jambo hili na liwe faraja yenu.
3 Niacheni, nami pia nitanena;Tena nikiisha nena, zidini kudhihaki.
4 Mimi, je! Mashitaka yangu yamhusu mwanadamu?Nami kwa nini nisikose kusubiri?
5 Niangalieni, mkastaajabu,Mkaweke mkono kinywani.