13 Siku zao hutumia katika kufanikiwa,Kisha hushuka kuzimuni ghafula.
14 Walakini walimwambia Mungu. Tuondokee;Kwani hatutaki kuzijua njia zako.
15 Huyo Mwenyezi ni nani, hata tumtumikie?Nasi tutafaidiwa nini tukimwomba?
16 Tazama, kufanikiwa kwao hakumo mkononi mwao;Mashauri ya waovu na yawe mbali nami.
17 Je! Ni mara ngapi taa yao waovu huzimishwa?Na msiba wao kuwajilia?Na Mungu kuwagawanyia uchungu kwa hasira yake?
18 Ili wawe kama mabua makavu mbele ya upepo,Kama makapi yaliyochukuliwa na dhoruba?
19 Mwasema, Mungu huwawekea watoto wa mtu huo uovu wake.Na amlipe mwenyewe, ili apate kuujua.