20 Macho yake mwenyewe na yaone uharibifu wake,Akanywe ghadhabu zake Mwenyezi.
21 Kwani ana furaha gani katika mbari yake baada yake,Hesabu ya miezi yake itakapokwisha katwa katikati?
22 Je! Mtu awaye yote atamfundisha Mungu maarifa?Naye ndiye awahukumuye walioko juu.
23 Mmoja hufa katika nguvu zake kamili,Mwenye kukaa salama na kustarehe;
24 Vyombo vyake vimejaa maziwa,Na mafuta ya mifupani mwake ni laini.
25 Mwingine hufa katika uchungu wa roho,Asionje mema kamwe.
26 Wao hulala mavumbini sawasawa,Mabuu huwafunika.