27 Tazama, nayajua mawazo yenu,Na mashauri mnayoazimia kwa uovu juu yangu.
28 Kwa kuwa mwasema, Nyumba ya huyo mkuu i wapi?Na hema waliyoikaa hao waovu i wapi?
29 Je! Hamkuwauliza wapitao njiani?Na maonyo yao hamyajui?
30 Kwamba mwovu huachiliwa katika siku ya msiba?Na kuongozwa nje katika siku ya ghadhabu?
31 Ni nani atakayetangaza njia yake usoni pake?Tena ni nani atakayemlipa kwa hayo aliyofanya?
32 Pamoja na hayo atachukuliwa kaburini,Nao watalinda zamu juu ya ziara lake.
33 Udongo wa bondeni utakuwa tamu kwake,Na watu wote watafuata nyuma yake,Kama vile walivyomtangulia watu wasiohesabika.