5 Niangalieni, mkastaajabu,Mkaweke mkono kinywani.
6 Hata nikumbukapo nahuzunika,Na utisho wanishika mwilini mwangu.
7 Mbona waovu wanaishi,Na kuwa wazee, naam, na kuongezeka kuwa na nguvu?
8 Kizazi chao kinathibitika nao machoni pao,Na wazao wao mbele ya macho yao.
9 Nyumba zao zi salama pasina hofu,Wala fimbo ya Mungu haiwapigi.
10 Fahali wao huvyaza wala hapungukiwi na nguvu;Ng’ombe wao mke huzaa, asiharibu mimba.
11 Huwatoa kama kundi watoto wao.Na watoto wao hucheza.