7 Mbona waovu wanaishi,Na kuwa wazee, naam, na kuongezeka kuwa na nguvu?
8 Kizazi chao kinathibitika nao machoni pao,Na wazao wao mbele ya macho yao.
9 Nyumba zao zi salama pasina hofu,Wala fimbo ya Mungu haiwapigi.
10 Fahali wao huvyaza wala hapungukiwi na nguvu;Ng’ombe wao mke huzaa, asiharibu mimba.
11 Huwatoa kama kundi watoto wao.Na watoto wao hucheza.
12 Huimba kwa matari na kwa kinubi,Na kuifurahia sauti ya filimbi.
13 Siku zao hutumia katika kufanikiwa,Kisha hushuka kuzimuni ghafula.