9 Nyumba zao zi salama pasina hofu,Wala fimbo ya Mungu haiwapigi.
10 Fahali wao huvyaza wala hapungukiwi na nguvu;Ng’ombe wao mke huzaa, asiharibu mimba.
11 Huwatoa kama kundi watoto wao.Na watoto wao hucheza.
12 Huimba kwa matari na kwa kinubi,Na kuifurahia sauti ya filimbi.
13 Siku zao hutumia katika kufanikiwa,Kisha hushuka kuzimuni ghafula.
14 Walakini walimwambia Mungu. Tuondokee;Kwani hatutaki kuzijua njia zako.
15 Huyo Mwenyezi ni nani, hata tumtumikie?Nasi tutafaidiwa nini tukimwomba?