1 Ndipo huyo Elifazi Mtemani akajibu, na kusema,
2 Je! Yumkini mtu awaye yote kumfaa Mungu?Hakika yeye aliye na hekima hujifaa mwenyewe.
3 Je! Mwenyezi hupata furaha katika wewe kuwa mwenye haki?Au je, ni faida kwake, kwamba wafanya njia zako kuwa timilifu?
4 Je! Ni kwa wewe kumcha yeye anakukemea?Na kuingia hukumuni nawe?
5 Je! Uovu wako si mkuu?Wala maovu yako hayana mwisho.
6 Kwa kuwa umetwaa dhamana kwa nduguyo bure,Na kuwavua nguo zao walio uchi.
7 Hukumpa maji ya kunywa huyo aliyechoka,Nawe umemnyima chakula huyo mwenye njaa.