16 Ambao walinyakuliwa kabla ya wakati wao,Msingi wao ulimwagika kama kijito cha maji;
17 Waliomwambia Mungu, Tuondokee;Tena, Huyo Mwenyezi aweza kutufanyia nini?
18 Naye ndiye aliyezijaza nyumba zao vitu vyema;Lakini mashauri ya waovu na yawe mbali nami.
19 Wenye haki huyaona hayo wakafurahi;Nao wasio na hatia huwacheka;
20 Wasema, Hakika hao waliotuinukia wamekatiliwa mbali,Na mabaki yao moto umeyateketeza.
21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani;Ndivyo mema yatakavyokujia.
22 Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake,Na maneno yake yaweke moyoni mwako.