22 Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake,Na maneno yake yaweke moyoni mwako.
23 Ukimrudia Mwenyezi, utajengwa;Ukiuondoa udhalimu mbali na hema yako.
24 Nawe hazina zako ziweke mchangani,Na dhahabu ya Ofiri iweke kati ya mawe ya vijito;
25 Naye Mwenyezi atakuwa hazina yako,Atakuwa ni fedha ya thamani kwako.
26 Kwani ndipo utakapojifurahisha katika Mwenyezi,Na kuinua uso wako kumwelekea Mungu.
27 Utamwomba yeye naye atakusikia;Nawe utazitimiliza nadhiri zako.
28 Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako;Na mwanga utaziangazia njia zako.