25 Naye Mwenyezi atakuwa hazina yako,Atakuwa ni fedha ya thamani kwako.
26 Kwani ndipo utakapojifurahisha katika Mwenyezi,Na kuinua uso wako kumwelekea Mungu.
27 Utamwomba yeye naye atakusikia;Nawe utazitimiliza nadhiri zako.
28 Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako;Na mwanga utaziangazia njia zako.
29 Hapo watakapokuangusha, utasema, Kuna kuinuka tena;Naye mnyenyekevu Mungu atamwokoa.
30 Atamwokoa na huyo asiye na hatia;Naam, utaokolewa kwa sababu ya usafi wa mikono yako.