1 Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,
2 Jinsi ulivyomsaidia huyo asiye na uwezo!Jinsi ulivyouokoa mkono usio na nguvu!
3 Jinsi ulivyomshauri huyo asiye na hekima!Na kutangaza ujuzi wa kweli kwa wingi!
4 Je! Umetamka maneno kwa nani?Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako?