3 Jinsi ulivyomshauri huyo asiye na hekima!Na kutangaza ujuzi wa kweli kwa wingi!
4 Je! Umetamka maneno kwa nani?Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako?
5 Hao waliokufa watetemaChini ya maji na hao wayakaao.
6 Kaburi li wazi mbele yake,Uharibifu nao hauna kifuniko.
7 Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu,Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu.
8 Huyafunga maji ndani ya mawingu yake mazito;Na hilo wingu halipasuki chini yake.
9 Husitiri uso wa kiti chake cha enzi,Na kulitandaza wingu lake juu yake.