3 (Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu,Na roho ya Mungu i katika pua yangu;)
4 Hakika midomo yangu haitanena yasiyo haki,Wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.
5 Hasha! Nisiwahesabie ninyi kuwa na haki;Hata nitakapokufa sitajiondolea uelekevu wangu.
6 Haki yangu naishika sana, wala sitaiacha;Moyo wangu hautanisuta wakati nikiwapo hai.
7 Adui yangu na awe kama huyo mwovu,Na mwenye kuondoka kinyume changu na awe kama asiye haki.
8 Kwani tumaini la mpotovu ni nini, ingawa ajipatia faida,Hapo Mungu amwondoleapo roho yake?
9 Je! Mungu atakisikia kilio chake,Taabu zitakapomfikilia?