9 Je! Mungu atakisikia kilio chake,Taabu zitakapomfikilia?
10 Je! Atajifurahisha katika Mwenyezi,Na kumlingana Mungu nyakati zote?
11 Nitawafundisha ninyi mambo ya mkono wa Mungu;Hayo yaliyo kwa Mwenyezi sitayaficha.
12 Tazama, ninyi nyote mmeyaona wenyewe;Mbona basi mmebatilika kabisa?
13 Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu kwa Mungu,Na urithi wa hao waoneao, waupokeao kwa Mwenyezi.
14 Watoto wake wakiongezeka ni kwa upanga;Na wazao wake hawatashiba chakula.
15 Hao watakaosalia kwake watazikwa katika kufa,Wala wajane wake waliofiwa na waume hawataomboleza.