1 Hakika kuna shimo wachimbako fedha,Na mahali wapatapo dhahabu waisafishayo.
2 Chuma hufukuliwa katika ardhi,Na shaba huyeyushwa katika mawe.
3 Binadamu hukomesha giza;Huyatafuta-tafuta hata mpaka ulio mbali,Mawe ya giza kuu, giza tupu.
4 Hufukua shimo mbali na makao ya watu;Husahauliwa na nyayo zipitazo;Huning’inia mbali na watu, huyumba-yumba huko na huko.
5 Katika ardhi ndimo kitokeamo chakula;Na chini yake hupinduliwa kama kwa moto.
6 Mawe yake ni mahali zipatikanapo yakuti;Nayo ina mchanga wa dhahabu.