10 Hukata mifereji kati ya majabali;Na jicho lake huona kila kito cha thamani
11 Hufunga vijito visichuruzike;Na kitu kilichostirika hukifunua.
12 Bali hekima itapatikana wapi?Na mahali pa ufahamu ni wapi?
13 Mwanadamu hajui thamani yake,Wala haionekani katika nchi ya walio hai.
14 Vilindi vyasema, Haimo ndani yangu;Na bahari yasema, Haiko kwangu.
15 Haipatikani kwa dhahabu,Wala fedha haitapimwa iwe thamani yake.
16 Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri,Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti ya samawi.