16 Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri,Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti ya samawi.
17 Dhahabu na vioo haviwezi kulinganishwa nayo;Wala kubadili kwake hakutakuwa kwa vyombo vya dhahabu safi.
18 Havitatajwa fedhaluka wala bilauri;Naam, kima cha hekima chapita marijani.
19 Yakuti ya rangi ya manjano ya Kushi haitasawazishwa nayo,Wala haitatiwa kima kwa dhahabu safi.
20 Basi hekima yatoka wapi?Na mahali pa ufahamu ni wapi?
21 Kwa kuwa imefichwa mbali na macho ya wote walio hai,Na kusitirika na ndege wa angani.
22 Uharibifu na Mauti husema,Tumesikia habari zake kwa masikio yetu.