22 Uharibifu na Mauti husema,Tumesikia habari zake kwa masikio yetu.
23 Mungu ndiye aijuaye njia yake,Naye anajua mahali pake.
24 Maana anatazama hata miisho ya nchi,Na kuona chini ya mbingu nzima.
25 Apate kuufanyia upepo uzito wake;Naam, anayapima maji kwa kipimo.
26 Hapo alipoiwekea mvua amri,Na njia kwa umeme wa radi.
27 Ndipo alipoiona na kuitangaza;Aliithibitisha, naam, na kuichunguza.
28 Kisha akamwambia mwanadamu,Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima,Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.