24 Maana anatazama hata miisho ya nchi,Na kuona chini ya mbingu nzima.
25 Apate kuufanyia upepo uzito wake;Naam, anayapima maji kwa kipimo.
26 Hapo alipoiwekea mvua amri,Na njia kwa umeme wa radi.
27 Ndipo alipoiona na kuitangaza;Aliithibitisha, naam, na kuichunguza.
28 Kisha akamwambia mwanadamu,Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima,Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.