3 Binadamu hukomesha giza;Huyatafuta-tafuta hata mpaka ulio mbali,Mawe ya giza kuu, giza tupu.
4 Hufukua shimo mbali na makao ya watu;Husahauliwa na nyayo zipitazo;Huning’inia mbali na watu, huyumba-yumba huko na huko.
5 Katika ardhi ndimo kitokeamo chakula;Na chini yake hupinduliwa kama kwa moto.
6 Mawe yake ni mahali zipatikanapo yakuti;Nayo ina mchanga wa dhahabu.
7 Njia ile hapana ndege mkali aijuaye,Wala jicho la tai halijaiona;
8 Wanyama wakali wajivunao hawajaikanyaga,Wala simba mkali hajaipita.
9 Huunyoshea mwamba wa gumegume mkono wake;Huipindua milima hata misingi yake.