6 Mawe yake ni mahali zipatikanapo yakuti;Nayo ina mchanga wa dhahabu.
7 Njia ile hapana ndege mkali aijuaye,Wala jicho la tai halijaiona;
8 Wanyama wakali wajivunao hawajaikanyaga,Wala simba mkali hajaipita.
9 Huunyoshea mwamba wa gumegume mkono wake;Huipindua milima hata misingi yake.
10 Hukata mifereji kati ya majabali;Na jicho lake huona kila kito cha thamani
11 Hufunga vijito visichuruzike;Na kitu kilichostirika hukifunua.
12 Bali hekima itapatikana wapi?Na mahali pa ufahamu ni wapi?