8 Wanyama wakali wajivunao hawajaikanyaga,Wala simba mkali hajaipita.
9 Huunyoshea mwamba wa gumegume mkono wake;Huipindua milima hata misingi yake.
10 Hukata mifereji kati ya majabali;Na jicho lake huona kila kito cha thamani
11 Hufunga vijito visichuruzike;Na kitu kilichostirika hukifunua.
12 Bali hekima itapatikana wapi?Na mahali pa ufahamu ni wapi?
13 Mwanadamu hajui thamani yake,Wala haionekani katika nchi ya walio hai.
14 Vilindi vyasema, Haimo ndani yangu;Na bahari yasema, Haiko kwangu.