16 Nalikuwa baba kwa mhitaji,Na daawa ya mtu nisiyemjua naliichunguza.
17 Nami nilizivunja taya za wasio haki,Na kumpokonya mawindo katika meno yake.
18 Ndipo niliposema, Nitakufa ndani ya kioto changu,Nami nitaziongeza siku zangu kama mchanga;
19 Shina langu limeenea hata kufika majini,Na umande hukaa usiku kucha katika matawi yangu;
20 Utukufu wangu utakuwa mpya kwangu,Na uta wangu hurejezwa upya mkononi mwangu.
21 Watu walitega masikio kunisikiliza, na kungoja,Wakanyamaa kimya wapate sikia mashauri yangu.
22 Hawakunena tena baada ya kusikia maneno yangu;Matamko yangu yakadondoka juu yao.