7 Wakati nilipotoka kwenda mjini, hata langoni,Nilipokitengeza kiti changu katika njia kuu,
8 Hao vijana waliniona wakajificha,Nao wazee wakaniondokea na kusimama;
9 Wakuu wakanyamaa wasinene,Na kuweka mikono yao vinywani mwao;
10 Sauti yao masheki ilinyamaa,Na ndimi zao zilishikamana na makaakaa yao.
11 Maana sikio liliponisikia, ndipo likanibarikia;Na jicho liliponiona, likanishuhudia.
12 Kwa sababu nalimwokoa maskini aliyenililia;Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia.
13 Baraka yake yeye aliyekuwa karibu na kupotea ilinijia;Nikaufanya moyo wa mjane kuimba kwa furaha.