1 Baada ya hayo Ayubu akafunua kinywa chake, na kuilaani siku yake.
2 Ayubu akajibu, na kusema;
3 Na ipotelee mbali ile siku niliyozaliwa mimi,Na ule usiku uliosema,Mtoto mume ametungishwa mimba.
4 Siku hiyo na iwe giza;Mungu asiiangalie toka juu,Wala mwanga usiiangazie.
5 Ishikwe na giza, giza tupu, kuwa yake;Wingu na likae juu yake;Chote kiifanyacho siku kuwa giza na kiitishe.
6 Tena usiku huo, na ushikwe na giza kuu;Usihesabiwe katika siku za mwaka;Wala kutiwa katika hesabu ya miezi.
7 Tazama, usiku huo na uwe tasa;Wala isiwe ndani yake sauti ya shangwe.