11 Mbona si kufa mimi tokea mimbani?Mbona nisitoe roho hapo nilipotoka tumboni?
12 Mbona hayo magoti kunipokea?Au hayo maziwa, hata nikanyonya?
13 Maana hapo ningelala na kutulia;Ningelala usingizi; na kupata kupumzika;
14 Pamoja na wafalme na washauri wa dunia,Hao waliojijengea maganjoni;
15 Au pamoja na wakuu wenye dhahabu,Waliozijaza fedha nyumba zao;
16 Au, kama kuzikwa mimba iliyoharibika, nisingekuwako;Kama wachanga wasiouona mwanga kabisa.
17 Huko waovu huacha kusumbua;Huko nako hao waliochoka wapumzika