13 Maana hapo ningelala na kutulia;Ningelala usingizi; na kupata kupumzika;
14 Pamoja na wafalme na washauri wa dunia,Hao waliojijengea maganjoni;
15 Au pamoja na wakuu wenye dhahabu,Waliozijaza fedha nyumba zao;
16 Au, kama kuzikwa mimba iliyoharibika, nisingekuwako;Kama wachanga wasiouona mwanga kabisa.
17 Huko waovu huacha kusumbua;Huko nako hao waliochoka wapumzika
18 Huko wafungwa waona raha pamoja;Hawaisikii sauti yake msimamizi.
19 Wakuu na wadogo wako huko;Mtumishi yu huru kwa bwana wake.