16 Au, kama kuzikwa mimba iliyoharibika, nisingekuwako;Kama wachanga wasiouona mwanga kabisa.
17 Huko waovu huacha kusumbua;Huko nako hao waliochoka wapumzika
18 Huko wafungwa waona raha pamoja;Hawaisikii sauti yake msimamizi.
19 Wakuu na wadogo wako huko;Mtumishi yu huru kwa bwana wake.
20 Mbona yeye aliye mashakani kupewa mwanga,Na hao wenye uchungu rohoni kupewa uhai;
21 Ambao wangojea mauti, lakini hawayapati;Na kuyachimbulia zaidi ya kutafuta hazina iliyostirika;
22 Ambao wafurahi mno,Na kushangilia watakapoliona kaburi?