4 Siku hiyo na iwe giza;Mungu asiiangalie toka juu,Wala mwanga usiiangazie.
5 Ishikwe na giza, giza tupu, kuwa yake;Wingu na likae juu yake;Chote kiifanyacho siku kuwa giza na kiitishe.
6 Tena usiku huo, na ushikwe na giza kuu;Usihesabiwe katika siku za mwaka;Wala kutiwa katika hesabu ya miezi.
7 Tazama, usiku huo na uwe tasa;Wala isiwe ndani yake sauti ya shangwe.
8 Na waulaani hao waulaanio mchana,Hao walio tayari kumwamsha huyo lewiathani.
9 Nyota za mapambazuko yake na ziwe giza;Na utafute mwanga lakini usiupate;Wala usiyaone makope ya asubuhi;
10 Kwa sababu haukuifunga milango ya tumbo la mamangu.Wala kunifichia taabu machoni.