12 Kwa mkono wangu wa kuume huinuka kundi;Huisukuma miguu yangu kando,Na kunipandishia njia zao za uharibifu.
13 Waiharibu njia yangu,Wauzidisha msiba wangu,Watu wasio na msaidizi.
14 Wanijilia kama wapitao katika ufa mpana;Katikati ya magofu wanishambulia.
15 Vitisho vimenigeukia;Huifukuza heshima yangu kama upepo;Na kufanikiwa kwangu kumepita kama wingu.
16 Sasa nafsi yangu inamwagika ndani yangu;Siku za mateso zimenishika.
17 Wakati wa usiku mifupa yangu huchomeka ndani yangu,Na maumivu yanayonitafuna hayapumziki.
18 Kwa ugonjwa wangu kuwa na nguvu nyingiMavazi yangu yameharibika;Hunikaza kama shingo ya kanzu yangu.