15 Vitisho vimenigeukia;Huifukuza heshima yangu kama upepo;Na kufanikiwa kwangu kumepita kama wingu.
16 Sasa nafsi yangu inamwagika ndani yangu;Siku za mateso zimenishika.
17 Wakati wa usiku mifupa yangu huchomeka ndani yangu,Na maumivu yanayonitafuna hayapumziki.
18 Kwa ugonjwa wangu kuwa na nguvu nyingiMavazi yangu yameharibika;Hunikaza kama shingo ya kanzu yangu.
19 Yeye amenibwaga topeni,Nami nimekuwa kama mavumbi na majivu.
20 Nakulilia wewe, wala huniitikii;Nasimama, nawe wanitazama tu.
21 Wewe umegeuka kuwa mkali kwangu;Nawe waniudhi kwa uweza wa mkono wako.