18 Kwa ugonjwa wangu kuwa na nguvu nyingiMavazi yangu yameharibika;Hunikaza kama shingo ya kanzu yangu.
19 Yeye amenibwaga topeni,Nami nimekuwa kama mavumbi na majivu.
20 Nakulilia wewe, wala huniitikii;Nasimama, nawe wanitazama tu.
21 Wewe umegeuka kuwa mkali kwangu;Nawe waniudhi kwa uweza wa mkono wako.
22 Waniinua juu hata upeponi, na kunipandisha juu yake;Nawe waniyeyusha katika dhoruba.
23 Kwani najua kuwa utanileta hata kifoni,Niifikilie nyumba waliyoandikiwa wenye uhai wote.
24 Je! Mtu katika kuanguka kwake hanyoshi mkono?Na kulilia msaada katika msiba wake?