19 Yeye amenibwaga topeni,Nami nimekuwa kama mavumbi na majivu.
20 Nakulilia wewe, wala huniitikii;Nasimama, nawe wanitazama tu.
21 Wewe umegeuka kuwa mkali kwangu;Nawe waniudhi kwa uweza wa mkono wako.
22 Waniinua juu hata upeponi, na kunipandisha juu yake;Nawe waniyeyusha katika dhoruba.
23 Kwani najua kuwa utanileta hata kifoni,Niifikilie nyumba waliyoandikiwa wenye uhai wote.
24 Je! Mtu katika kuanguka kwake hanyoshi mkono?Na kulilia msaada katika msiba wake?
25 Je! Mimi sikulia kwa ajili ya huyo aliyekuwa katika taabu?Nafsi yangu, je! Haikusononeka kwa ajili ya wahitaji?