27 Matumbo yangu yatokota, wala hayaachi;Siku za taabu zimenijilia.
28 Naenda nikiomboleza pasipo jua;Nasimama katika mkutano, na kuulilia msaada.
29 Mimi ni ndugu yao mbwa-mwitu,Ni mwenzao mbuni.
30 Ngozi yangu ni nyeusi, nayo yanitoka,Na mifupa yangu imeteketea kwa hari.
31 Kwa hiyo kinanda changu kimegeuzwa kuwa maombolezo,Na filimbi yangu kuwa sauti yao waliao.