5 Hufukuzwa watoke kati ya watu;Huwapigia kelele kama kumpigia mwivi.
6 Lazima hukaa katika mianya ya mabonde,Katika mashimo ya nchi na ya majabali.
7 Hulia kama punda vichakani;Hukusanyika chini ya upupu.
8 Wao ni wana wa wapumbavu, naam, watoto wa wahuni;Walifukuzwa kwa mijeledi watoke katika nchi.
9 Na sasa mimi nimekuwa wimbo wao,Naam, nimekuwa simo kwao.
10 Wao hunichukia, na kujitenga nami,Hawaachi kunitemea mate usoni.
11 Kwani ameilegeza kamba yake, na kunitesa,Wala hawajizuii tena mbele yangu.