1 Nilifanya agano na macho yangu;Basi nawezaje kumwangalia msichana?
2 Kwani sehemu ya Mungu itokayo juu ingekuwa nini,Na urithi wa Mwenyezi utokao juu?
3 Je! Siyo msiba kwa wasio haki,Na hasara kwao watendao uovu?
4 Je! Yeye hazioni njia zangu,Na kuzihesabu hatua zangu zote?
5 Kwamba nimetembea katika ubatili,Na mguu wangu umeukimbilia udanganyifu;