15 Je! Huyo aliyenifanya mimi ndani ya tumbo, siye aliyemfanya na yeye?Si yeye mmoja aliyetufinyanga tumboni?
16 Ikiwa nimewanyima maskini haja zao,Au kama nimeyatia kiwi macho ya mwanamke mjane;
17 Au kama nimekula tonge langu peke yangu,Mayatima wasipate kulila;
18 (La, tangu ujana wangu alikua pamoja nami kama kwa baba;Nami nimekuwa ni kiongozi cha mjane tangu tumbo la mamangu);
19 Ikiwa nimemwona mtu kuangamia kwa kukosa nguo,Au wahitaji kukosa mavazi;
20 Ikiwa viuno vyake havikunibarikia,Au kama hakupata moto kwa manyoya ya kondoo zangu;
21 Ikiwa nimewainulia mayatima mkono,Nilipoona msaada wangu langoni;