23 Kwani msiba utokao kwa Mungu ulikuwa na kitisho kwangu,Na kwa sababu ya ukuu wake sikuweza kufanya neno.
24 Ikiwa nimeifanya dhahabu kuwa tumaini langu,Na kuiambia dhahabu safi, Wewe u tegemeo langu;
25 Kama nilifurahi kwa kuwa mali yangu yalikuwa mengi,Na kwa sababu mkono wangu umepata vitu vingi;
26 Kama nililitazama jua lilipoangaza,Au mwezi ukiendelea katika kung’aa;
27 Na moyo wangu umeshawishwa kwa siri,Na midomo yangu imeubusu mkono wangu;
28 Hilo nalo lingekuwa uovu wa kuadhibiwa na waamuzi;Kwani ningemwambia uongo Mungu aliye juu.
29 Kama nilifurahi kwa kuangamia kwake huyo aliyenichukia,Au kujitukuza alipopatikana na maovu;