27 Na moyo wangu umeshawishwa kwa siri,Na midomo yangu imeubusu mkono wangu;
28 Hilo nalo lingekuwa uovu wa kuadhibiwa na waamuzi;Kwani ningemwambia uongo Mungu aliye juu.
29 Kama nilifurahi kwa kuangamia kwake huyo aliyenichukia,Au kujitukuza alipopatikana na maovu;
30 (Naam, sikukiacha kinywa changu kufanya dhambiKwa kuutaka uhai wake kwa kuapiza);
31 Kama watu wa hemani mwangu hawakunena,Ni nani awezaye kumpata mtu asiyeshibishwa na yeye kwa nyama?
32 Mgeni hakulala njiani;Lakini nilimfungulia msafiri milango yangu;
33 Ikiwa kama mwanadamu nimeyafunika makosa yangu,Kwa kuuficha uovu wangu kifuani mwangu;