32 Mgeni hakulala njiani;Lakini nilimfungulia msafiri milango yangu;
33 Ikiwa kama mwanadamu nimeyafunika makosa yangu,Kwa kuuficha uovu wangu kifuani mwangu;
34 Kwa sababu niliwaogopa mkutano mkubwa,Na dharau la jamaa lilinitia hofu,Hata nilinyamaa kimya, nisitoke mlangoni-
35 Laiti ningekuwa na mtu wa kunisikia!(Tazama, sahihi yangu ni hii, Mwenyezi na anijibu);Laiti ningekuwa na hayo mashitaka yaliyoandikwa na adui yangu!
36 Hakika ningeyachukua mabegani;Ningejifungia mfano wa kilemba.
37 Ningemwambia hesabu ya hatua zanguNingemkaribia kama vile mkuu.
38 Kama nchi yangu yalia juu yangu,Na matuta yake hulia pamoja;