5 Kwamba nimetembea katika ubatili,Na mguu wangu umeukimbilia udanganyifu;
6 (Na nipimwe katika mizani iliyo sawasawa,Ili Mungu aujue uelekevu wangu);
7 Kwamba hatua yangu imekengeuka na kuiacha njia,Na moyo wangu kuyaandama macho yangu,Tena kwamba kipaku cho chote kimeshikamana na mikono yangu;
8 Basi na nipande, mwingine ale;Naam, mazao ya shamba langu na yang’olewe.
9 Kama moyo wangu ulishawishwa kwa mwanamke,Nami nimeotea mlangoni pa jirani yangu;
10 Ndipo hapo mke wangu na asage kwa mwingine,Na wengine na wainame juu yake.
11 Kwani hilo lingekuwa kosa kuu;Naam, lingekuwa ni uovu wa kuadhibiwa na waamuzi;