8 Basi na nipande, mwingine ale;Naam, mazao ya shamba langu na yang’olewe.
9 Kama moyo wangu ulishawishwa kwa mwanamke,Nami nimeotea mlangoni pa jirani yangu;
10 Ndipo hapo mke wangu na asage kwa mwingine,Na wengine na wainame juu yake.
11 Kwani hilo lingekuwa kosa kuu;Naam, lingekuwa ni uovu wa kuadhibiwa na waamuzi;
12 Kwa kuwa ni moto uteketezao hata Uharibifu,Nao ungeyang’oa maongeo yangu yote.
13 Kama nimeidharau daawa ya mtumishi wangu, au ya kijakazi changu,Waliposhindana nami;
14 Basi Mungu atakapoinuka nitafanya nini?Naye atakapozuru, nitamjibuje?