13 Jitunzeni msiseme, Sisi tumepata hekima;Mungu yumkini akamshinda, si mtu;
14 Kwa kuwa yeye hajayaelekeza maneno yake kwangu;Wala sitamjibu mimi kwa maneno yenu.
15 Wameshangaa, hawajibu tena;Hawana neno la kusema.
16 Na mimi, je! Ningoje, kwa sababu hawaneni,Kwa sababu wasimama kimya, wala wasijibu tena;
17 Mimi nami nitajibu sehemu yangu,Mimi nami nitaonyesha nionavyo.
18 Kwa kuwa nimejaa maneno;Roho iliyo ndani yangu hunihimiza.
19 Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa;Kama viriba vipya li karibu na kupasuka.