15 Wameshangaa, hawajibu tena;Hawana neno la kusema.
16 Na mimi, je! Ningoje, kwa sababu hawaneni,Kwa sababu wasimama kimya, wala wasijibu tena;
17 Mimi nami nitajibu sehemu yangu,Mimi nami nitaonyesha nionavyo.
18 Kwa kuwa nimejaa maneno;Roho iliyo ndani yangu hunihimiza.
19 Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa;Kama viriba vipya li karibu na kupasuka.
20 Nitanena, ili nipate kutulia;Nitafunua midomo yangu na kujibu.
21 Tafadhali, nisiupendelee uso wa mtu;Wala sitajipendekeza kwa mtu ye yote.