18 Kwa kuwa nimejaa maneno;Roho iliyo ndani yangu hunihimiza.
19 Tazama, tumbo langu ni kama divai iliyozibwa;Kama viriba vipya li karibu na kupasuka.
20 Nitanena, ili nipate kutulia;Nitafunua midomo yangu na kujibu.
21 Tafadhali, nisiupendelee uso wa mtu;Wala sitajipendekeza kwa mtu ye yote.
22 Kwani mimi sijui kujipendekeza;Au Muumba wangu angeniondoa kwa upesi.