6 Basi Elihu mwana wa Barakeli, Mbuzi, akajibu, na kusema,Mimi ni kijana, na ninyi ni wazee sana;Kwa hiyo nilijizuia, nisithubutu kuwaonyesha nionavyo.
7 Nilisema, Yafaa siku ziseme,Na wingi wa miaka ufundishe hekima.
8 Lakini imo roho ndani ya mwanadamu,Na pumzi za Mwenyezi huwapa akili.
9 Sio wakuu walio wenye akili,Wala sio wazee watambuao hukumu.
10 Basi nilisema, Nisikilizeni mimi;Mimi nami nitawaonyesha nionavyo.
11 Tazama, niliyangojea maneno yenu,Nilizisikiliza nisikie hoja zenu,Hapo mlipokitafuta mtakalonena.
12 Naam, niliwasikiza ninyi,Na tazama, hapana mmoja aliyemshinda Ayubu,Wala kumjibu maneno yake, kati yenu.